“Tanzania haina UDIKTETA”- AG
Mwanasheria mkuu wa Tanzania George Masaju.
Mwanasheria mkuu wa Tanzania Ndg. George Masaju, amesema kuwa nchi hii inatawaliwa kwa kuzingatia mgawanyo wa madaraka na kwamba kila muhimili wa dola unatekeleza majukumu yake hivyo hakuna usahihi wowote pale baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaposema nchi inautawala wa kidikteta.
Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu jijini Dar Es Salaam, Masaju amewataka wanasiasa watii vyombo vya dola likiwemo jeshi la polisi pamoja na mahakama, huku akitoa wito wa kutofanya maandamano ya ‘UKUTA’ siku ya Septemba 1 kwakuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ilishawapa ushauri wa kutofanya hivyo kwa sababu hakuna utawala wa kidikteta nchini.
Aidha mwanasheria huyo amesisitiza pia wanasiasa kutotumia maneno ya kichochezi ambayo yanavuruga Amani na Usalama wa nchi.
Aidha mwanasheria huyo amesisitiza pia wanasiasa kutotumia maneno ya kichochezi ambayo yanavuruga Amani na Usalama wa nchi.

No comments: